Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (A.S) - ABNA -, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araqchi ameeleza matokeo ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani katika mkutano wake na Waandishi wa Habari leo mwishoni mwa mazungumzo ya Roma. Alisema katika suala hili: "Tulikuwa na mazungumzo ya saa nne, na wakati huu, katika mwendelezo wa mkutano uliopita, mkutano huu umekuwa mkutano mzuri na mazungumzo ya mapatano yanaendelea." Mazungumzo ya Roma yalifanyika katika mazingira yenye kujenga na yanaendelea mbele, na sisi tunasonga mbele. Wakati huu, tulifaulu kufikia uelewano mzuri zaidi kuhusu kanuni na malengo, na ilikubaliwa kuwa mazungumzo yaendelee na kuingia katika awamu inayofuata ya kiufundi.
Araqchi, akitangaza kuendelea kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani ameongeza kuwa: "Kwa hivyo, mazungumzo ya kiufundi katika ngazi ya wataalamu yataanza nchini Oman Jumatano ya wiki hii, na kwa kawaida, wataalamu watakuwa na muda zaidi wa kueleza kwa kina na kubuni mfumo wa makubaliano. Tutakutana tena Jumamosi ijayo nchini Oman na kupitia upya matokeo ya kazi ya wataalamu."
Amebainisha: Kiongozi Muadhamu pia alisema mazungumzo hayo ni miongoni mwa kazi za Wizara ya Mambo ya Nje na yatafanyika kwa utulivu na umakini. Bila shaka, hakuna sababu ya kuwa na matumaini mengi. Lazima tuwe waangalifu sana. Kwa upande mwingine, hakuna sababu ya kukata tamaa kupita kiasi. Natumai tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi wiki ijayo baada ya mikutano ya kiufundi.
Your Comment